Wednesday, June 24, 2015

MWEZI MTUKUFU WAMUOKOA MTUHUMIWA WA WIZI

IMG_0581Kibaka aliyejulikana kama Baba Hawa, mkazi wa Sinza Kamanyola jijini Dar akipokea kipigo kikali toka kwa wananchi wenye hasira baada ya kunaswa akiiba kinyonyeo cha kompyuta (flash) kwenye duka moja la vifaa vya ofisini (stationery) lililopo Bamaga, Mwenge.
Chande Abdallah
Bahati ilioje! Kibaka mmoja aliyejulikana kama Baba Hawa, mkazi wa Sinza Kamanyola jijini Dar juzikati nusura auawe kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira baada ya kunaswa akiiba kinyonyeo cha kompyuta (flash) kwenye duka moja la vifaa vya ofisini (stationery) lililopo Bamaga, Mwenge.
IMG_0574Kibaka huyo akiendelea kupokea ‘dozi’.
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa duka hilo, mtu huyo aliingia kwa mbwembwe kama mteja wa kawaida akiomba kutolewa fotokopi ya makaratasi yake ambayo yalionesha mahesabu ya chuo kikuu.
IMG_0567…Akiwa hoi taabani baada ya kutembezewa kichapo.
Wakiongea kwa kupokezana, wafanyakazi hao walidai wakati wakimhudumia, alionekana kuwa macho juujuu huku akishtuka kila alipotazamwa, jambo lililowafanya wamtilie mashaka hivyo kukagua vifaa vyao.
IMG_0552…Akishughulikiwa sawasawa na wananchi wenyw hasira kali.
Baada ya kuangalia pale juu nikagundua flashi kama tano hivi hazipo, ndiyo nikamtaka huyo mkaka afungue begi lake, na kweli nikamkuta nazo akiwa ameziweka humo ndani, alisema mmoja wa wafanyakazi wa duka hilo na kuongeza kuwa alipodaiwa fedha za fotokopi, hakuwa nazo jambo lililoashiria kuwa alienda pale kwa lengo la kuiba tu hivyo kumwitia mwizi.
IMG_0543Baba hawa akihojiwa na wananchi waliofika kwenye tukio hilo.
Wananchi wenye hasira walimzunguka haraka na kuanza kumdondoshea kipigo kikali kilichomfanya alie na kuomba msamaha kwa kupitiwa na shetani kwani alikuwa amefunga.
IMG_0557Baadhi ya vitu alivyokuwa ameiba na kutunza kwenye begi.
Kwa maneno hayo, kutokana na heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wananchi hao waliingia huruma, kwani badala ya kumtia moto kama walivyotaka, wakaamua kumpa adhabu ya kumchapa viboko kwa kutumia magongo ya mifagio mpaka walipotosheka na kumuacha aondoke zake baada ya kurudisha alivyoiba.
Mwizi huyo aliwashukuru kwa kumnusuru na kifo huku akiondoka eneo hilo kuelekea kusikojulikana.