Wednesday, June 24, 2015

DOKTA FADHILI AMPA ZARI ZAWADI YA BAISKELI

DOKTA FADHILI AMZAWADIA ZARI BAISKELI (2)Mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Mwandishi wetu
DAKTARI wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asili kilichopo Mbezi-Afrikana, Dokta Fadhili Emily, amemnunulia baiskeli ya kubebea mtoto, mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kama zawadi pindi atakapojifungua.
DOKTA FADHILI AMZAWADIA ZARI BAISKELI (2)Mfano wa baiskeli aliyitoa Dkt. Fadhili kwa Zari.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko akiwa nchini Sweden alikoenda kwa ziara binafsi, Dokta Fadhili alisema kwa kutambua yeye ni mtu wa Kigoma anakotokea Diamond, ameona amnunulie shemeji yake huyo baiskeli hiyo ambayo kwa mujibu wake, ina thamani ya shilingi milioni 5 za Kitanzania.
DOKTA FADHILI AMZAWADIA ZARI BAISKELIDkt. Fadhili Emily.
“Mimi ni mwenyeji wa Kigoma, Zari ni shemeji yangu hivyo nikiwa huku Sweden nimeona niwawakilishe vijana wote wa kule kwa kumnunulia baiskeli hii ya kisasa shemeji yetu, wanatumia wanawake wengi Ulaya kubebea watoto wao,” alisema.
Zari anatarajiwa kujifungua kati ya Agosti au Septemba, mwaka huu ambapo ujio wa mtoto huyo umekuwa ukitengeneza vichwa vya habari kila kukicha