Wednesday, May 13, 2015

TYGA AHARIBU ‘BETHIDEI’ YA BLAC CHYNA

Rapa Tyga.
Los Angeles, Marekani
MODO Blac Chyna wikiendi iliyopita alisherehekea ‘bethidei’ yake kwa huzuni kufuatia kutokuwepo kwa aliyekuwa mpenzi wake, msanii Tyga.Chayna ambaye amezaa mtoto mmoja na rapa huyo, alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 27 kwa huzuni kubwa kutokana na kutokuwepo kwa mzazi mwenzake huyo.
Rapa Tyga akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Blac Chyna.
Chyna ambaye amepoteza penzi la Tyga, 25, na sasa anatoka na mrembo Kylie Jenner, 17, alishinda nyumbani akilia huku akisikiliza Wimbo wa You Use To Love Me uliombwa na Faith Evans.

Kwa mujibu wa chanzo, Chyna alimwambia rafiki yake:  “Zawadi ambayo ingekuwa kubwa kwangu ni kuhakikisha nakuwa na Tyga siku hiyo, nilitaka niwe naye kwenye boti tukisherehekea na mtoto wetu huku tukifungua shampeini na pia tukipata upepo wa bahari.”

Hata hivyo hivi karibuni bibi wa Tyga, Kim Nguyen, alipoulizwa nani anataka awe mkwe kati ya Kylie na Chyna alijibu: “Wote tunampenda Kylie, nafikiri ni vyema akiwa na Tyga.”