Friday, May 29, 2015

Video:Huwezi kuamini kama huu ni msiba, mke wa marehemu akavalishwa na shela kabisa

Bibi harusi
Sio tukio la kawaida kukutana na mtu kavaa gauni la harusi kwenye mazishi.. kwenye headlines za 254 jirani zetu wa nguvu Kenya kuna hii stori kutoka Kaunti ya Vihiga, unaambiwa mwanamke aliyefiwa na mume wake akalazimishwa kuvaa gauni ambalo anavaa bibi harusi wakati wa kufunga ndoa, alafu safari ya kwenda kwenye mazishi ikaanza.
Mary Akatsa ni kiongozi wa Kanisa la Jerusalem Church of Christ alikuwa akiongoza kila kitu mpaka mazishi yalipoisha, ukicheki kwenye hii video huyo mama anaonekana mkali hivi kama unaenda tofauti na maagizo yake.. wengine wanapigwa mpaka vibao.
Mazishi yalikuwa kama sherehe tu, kama ukiiona hii video unaweza kuhisi labda watu walikuwa kwenye harusi au sherehe nyingine ya kawaida.