MSANII mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amesema kuwa kwa sasa yupo katika kipindi kigumu cha upweke kutokana na mume wake kuhamishiwa Kisiwani Unguja kikazi.
Akizungumza na mwandishi wetu, Cathy alisema kuwa hakuna kitu kigumu na kinachomtesa kama kutenganishwa na mtu ambaye anampenda kwa dhati kwa sababu alimzoea kumuona kila siku lakini kwa sasa hadi apange safari ya kwenda kumuona.
“Mwenzako mapenzi ya mbali yananitesa sana kwa sababu nilishazoea kuwa na mume wangu wakati wote ndiyo maana sasa napata tabu mno japokuwa huwa nakwenda kumsalimia licha ya kuwa muoga sana wa maji,” alisema Cathy.