Alikiba, Bella pamoja na Aidan wakiwa ndani ya studio
“Nimefurahi jinsi tulivyoelewana masauti humu ndani,” amesema Bella.
“Nimemfanya sasa Alikiba kuimba na mimi akaonyesha kiwango kingine baada ya kukaa na king of the best melodies. Nilinyoosha melody na yeye ikabidi atembee vile vile, njia niliyopita mimi pick za juu sana na yeye akapita humo humo pia. Yaani imekuwa nzuri sana yaani kinoma. Kwahiyo ngoma ipo tayari,” ameongeza.
Hata hivyo muimbaji huyo amesema bado wimbo huo haujapewa jina.
“Jina na wimbo bado halijakamilika lakini baada ya leo ndo tutajua unaitwaje,” amesisitiza Bella.
“Sasa hivi tunajipanga kuhusu video na video ikikamilika baada ya mwezi wa ramadhani ngoma itatoka. Sitapenda ichelewe kwa sababu mashabiki walikuwa wanasumbua tufanye kolabo na Alikiba na ndo umefika muda wao kupata kile walichohitaji. Ingawa imechukua muda kutokana na sisi sote kuwa busy, kwahiyo mipango iliyobaki ni video ili tutoe video pamoja na audio na video tutafanya video kubwa kwa ufupi tu na sidhani kama tutashoot hapa nchini.”
Christian Bella aka King of the best melodies amedai kuwa kazi yake mpya na Alikiba itakuwa na utofauti mkubwa kwakuwa Kiba amebadilisha kwenye wimbo huo.
Akizungumza na Bongo5 leo, Bella amesema Kiba ni msanii aliyeweza kwenda naye sambamba kwenye kupanda na kushuka kwa sauti.“Nimefurahi jinsi tulivyoelewana masauti humu ndani,” amesema Bella.