Wema Abraham Sepetu ni mrembo mwenye headlines zake nyingi TZ kwa zaidi ya miaka 10… toka amekuwa Miss Tanzania, akaingia kwenye filamu na nyingine mpya kabisa ni safari yake kuingia kwenye headlines za siasa !!
Alikuwa LIVE kwenye show ya Clouds360 leo June 24 2015, mengine mapya kumi ambayo nimeyapata toka kwake ni haya hapa mtu wangu.
Unaijua ratiba yake ya kila siku; “Huwa naamka saa mbili au saa tatu inategemea na nini natakiwa kufanya siku hiyo… nafanya kazi za nyumbani kama mwanamke mwingine, napenda sana kupika. Nikiwa niko nyumbani sina kazi yoyote ninakaa na kupika.. kitu kinachochukua sana muda wangu ni shooting ya reality show na movie, sipendi sana kutokatoka”>>> Wema Sepetu.
Hii ndio sababu iliyomsukuma akaona agombee Ubunge; “Nimezaliwa kwenye siasa, Marehemu baba yangu alikuwa ni mwanasiasa, mama yangu ni mwanasiasa mpaka sasa hivi ni Mwenyekiti wa Serikali za mitaa. Marehemu baba yangu aliwahi kuniambia kwamba anatamani niingie kwenye siasa, mwaka 2010 nilikuwa siko tayari.. nimejisikia vibaya baba yangu amefariki wakati sijaonesha kwamba ninaweza kufanya, nina uhakika kule aliko anajisikia fahari”>>>