Huyu jamaa hajiiti Money Money bila sababu, pesa anazipata na bado anaendelea kuzipata. Mwaka huu kwa wana michezo waliolipwa pesa nyingi zaidi Mayweather ni namba moja kwa kuingiza dola milioni 300 kutokana na mahesabu ya Forbes.com
Floyd mwenye miaka 38 amemeenda kwenye makumbusho ya Mob huko Las Vegas ambapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya pesa nyingi alizoingiza mwaka huu ambazo ni dola milioni 300.
Kwenye maonyesho hayo ambapo wameweka pesa nyingi sana kwa na kuandika $300 Million Easy, Mayweather alifika na kupiga picha ya kumbukumbu akisema kwamba kuna nyingine nyingi zinakuja.
Kutokana na taarifa zake mwenyewe binafsi ni kwamba bado ana pambano lingine moja kabla hajamaliza career yake ya masumbwi.