Thursday, June 11, 2015

Kumbe umri sio Ishu, kikongwe wa miaka 100 na degree yake..

bibito
Kila mmoja anatambua kuwa elimu haina mwisho na kadri miaka inavyokwenda watu wengi wamekuwa wakitambua nini maana ya elimu huku wengi wao wakiamua kurudi darasani ili kujiongezea ujuzi zaidi.
bibi
Unamkumbuka yule kikongwe wa miaka 90 Priscilla Gogo huko Kenya aliyekuwa akisoma darasa la tano na wajuu zake wapatao sita? aliaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi duniani kusoma shule ya msingi.
kenya
Priscilla Gogo
Ukiachia stori hiyo wiki chache zilizopita huko Ujerumani kikongwe wa miaka 102 alihitimu PHD yake ya udaktari, Leo tena nimekusogezea ya bibi huyu Doreetha Daniel aliyeamua kuudhihirishia uma duniani baada ya kumaliza shahada yake kwenye chuo cha Canyons huko Santa Clarita, Carlifonia.
bibi2
Akiwa na miaka yake 99 alianza kuisaka safari yake ya elimu mwaka 2009 na kupania kupata degree yake kabla ya kutimiza miaka 100.
bbll
Bibi huyo amevunja rekodi katika chuo hicho kwakuwa mwanafunzi mzee zaidi tangu kuanzishwa kwa chuo hicho miaka 45 iliyopita.