Friday, June 19, 2015

MTOTO MZURI BATULI ACHEZEA SHARUBU ZA KAJALA!

Imelda Mtema 

STAA wa filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ameonekana kuchezea ‘sharubu’ za Kajala baada kuweka picha ya kiazi kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram kitu ambacho kimeonekana ni kumkejeli staa mwenzake huyo kutokana na Wema Sepetu kumuita kiazi. Staa wa filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’. Akichezesha taya na Amani baada ya kubanwa kwa nini aliweka picha hiyo kwenye Instagram yake, alisema kuwa yeye ana maamuzi ya kuweka kitu chochote kwenye ukurasa wake huo hivyo kama kuna mtu anajishtukia shauri yake.
Kwa upande wa Kajala alipoulizwa kama kuna tatizo lolote kati yake na Batuli alifunguka;
“Sijui kama mtu ana bifu na mimi basi ni yeye tu na kama mtu anaposti kitu kwa ajili ya kuniumiza naona ni kazi bure tu kwa kuwa vitu hivyo vinapita na maisha yanaendelea siku zote.”