Mpiganaji wa Al Shabaab, Thomas Evans aliyeuawa kwenye mapigano ya kundi hilo dhidi ya Jeshi la Kenya, anadaiwa kuwa raia wa Uingereza .
MWINGEREZA aliyebadili dini na kuwa Muislam, Thomas Evans, 25, ameuawa mwishoni mwa wiki akiwa anapigana na kundi la Al-Shaabab wakati likiendesha mapigano nchini Kenya.
Inaaminika mtu huyo kutoka High Wycombe, Buckinghamshire, Uingereza, alikuwa mmoja wa wapiganaji 11 waliouawa wakati waliposhambulia kituo kimoja cha jeshi kaskazini mwa Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Evans, alisilimu na kubadili jina lake na kuitwa Abdul Hakim na mnamo mwaka 2011, akiwa na umri wa miaka 19, Evans alijiunga na kundi hilo ambalo limesema lilifanya shambulio hilo Wilaya ya Lamu na “kuua askari wengi wa Kenya” lakini bila kutaja idadi ya wapiganaji wake waliouawa.
Wataalam wa serikali wanachunguza vinasaba vya mtu huyo kuhakikisha kama kweli ni yeye. Pia kuna mtu mwenye asili ya Kiarabu ambaye ni miongoni mwa waliokufa, mbali na wengine ambao wanaonekana ni wenye asili ya sehemu waliyouawa.
CREDIT DAILYMAIL