Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Wema Sepetu pamoja na kutengena na mpenzi wake Nassib Abdul ‘Diamond’ lakini alipoamua kutaja wasanii wanaofanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva mtaliki wake huyo kampa namba moja katika wasanii watano ambao yeye anaona wanafanya vizuri katika muziki.
“Muziki umeshika kasi na kuna wasanii ambao wanafanya vinzuri kuliko wengine, kwangu Top 5 yangu 1 Nassib, wa pili ni Ashley, Ali kiba, Barnaba na wa tano ni mirrow hawa ni wasanii wanzuri wapo level za kimataifa,”anasema Wema.
Aidha Wema amesema kwa upande wa wasanii wa kike anampenda sana mwimbaji Vanessa Mdee kwani anaimba na kucheza katika kiwango cha juu na kumfanya awe ni mpenzi wa kazi za msanii huyo, pia anataka watu wasimuelewe vibaya ni kwa mujibu wa mapenzi yake na maono yake