Saturday, June 20, 2015

Nora: Bongo Movie Wamesharibu Sanaa ya Uigizaji Tanzania...Huwezi Kaa na Wazazi Wako Ukaangalia Movie Wataharibu Hali ya Hewa tu

MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amedai kuwa ‘Bongo Movies’ wameharibu sanaa ya  uigizaji hapa Tanzania. Nora amefunguka hayo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao picha wa Instagram mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu akiwa lokesheni wakishuti movie.

"Naipenda kazi yangu na ninaiheshim sanaaaaa hii ndo sanaa ilionikuza mpaka leo na bado nakua nayo Mungu afungue heri zake lol tunajua kukomaaa ila nais Mungu ndo ameandika.

Nitatumia kipaji changu akili yangu kuwatumikia Watanzania pale palipokua apajaenda sawa nawaakikishia hiii kitu imewabeba wooooootee kiasi kwamba utatamani kumwita mama yako mnakaa mnajifunza kitu unakaa na baba yako mnaangalia sio kama movie nyingi zilizopo hukai na wazazi wako mkaangalia mana unajua wataharibu tuuuuu ila hii sio movie manaa bongo movie wamesharibu sanaa ya uigizaji tanzania," Nora ameandika.

Una maoni gani juu ya mtazamo huu wa Nora?