Tuesday, June 16, 2015

Team Diamond vs Team Alikiba: Kinachoendelea Instagram Kinatutia Aibu Watanzania!

Upinzani kati ya Diamond Platnumz na Alikiba sasa unaelekea kubaya. Kiukweli nimesikitishwa sana na kile ambacho ninakiona kikiendelea kwenye Instagram kati ya kambi hizi mbili.


Infact nahisi ushabiki huu una hasara nyingi kuliko faida kwenye industry yetu. Kwa leo sitaongelea jinsi ushabiki wa wasanii hawa wawili wenye nguvu unavyofanya wasanii wengine wanaofanya vizuri nchini kutoangaliwa, bali nitazungumzia kusikitishwa na kile kinachofanyika Instagram ambapo mashabiki wa Alikiba wameanzisha kampeni ya kuhakikisha kuwa Diamond anakosa tuzo kwenye MTV MAMA pamoja na mashabiki wa Diamond kumtukana Davido bila hatia!

Kwanini lakini tunafanya hivi? Hivi kweli tunaamua kujidhalilisha kiasi hiki? Majirani zetu wanatucheka, wanatubeza, wanatushangaa kweli kweli! Ushindani huu wa ndani kati ya wasanii hawa wawili kwanini uondoe utaifa wetu? Ushabiki gani huu?

Diamond Platnumz amechaguliwa kuwania vipengele vitatu kwenye tuzo za mwaka huu za MTV MAMA, iwapo akishinda, ushindi wake si wa familia yake na mashabiki wake peke yake, ni ushindi wa nchi nzima.
Kitendo kinachofanywa na maadui zake ambao infact ni mashabiki wa Alikiba na Wema Sepetu cha kuhamasishana kuwapigia kura Davido na Wizkid ili washinde na kumkomoa Diamond si kizuri.

Ni vyema linapokuja suala la kimataifa, tuweke tofauti zetu pembeni na tuwe kimoja. Kama hili haliwezekani, ni vyema kukaa tu kimya kuliko kuhamasishana kuwapigia kura wapinzani ili msanii wa Tanzania akose.

Haya, jana nimeshuhudia kitu kingine cha ajabu kabisa kwenye Instagram. Davido aliweka post kuonesha nominations nne alizopata.

From nowhere, comments nyingi zikawa ni kati ya Diamond vs Davido! Kwanini? Hii ni page ya msanii wa Nigeria ambaye anawataarifu mashabiki wake kuhusiana na nominations zake sasa huu ushabiki wa Diamond na yeye unatoka wapi tena?

Mbona tunatiana aibu kiasi hiki? Mbona tunaonekana malimbukeni na wageni wa mitandao? Hatuna kazi za kufanya ama nini hiki? Ndio, hadi wanaijeria wanatushangaa na kutuona kama wageni wa hivi vitu? Ugomvi wa Diamond na Davido ulishaisha siku nyingi sasa kwanini mashabiki wanalazimisha uendelee kuwepo?

Kama unampenda Diamond si unajua jinsi ya kumpigia kura, sasa kwanini uende kwenye page ya mtu ambaye wala hana time na masuala hayo na kuanza kumchafulia tu post yake?

Kiukweli tunatiana aibu. Tubadilike!

Bongo5