Wakazi wa vijiji vya Kapsina, Mona na Kiambirira kutoka katika kaunti ya Tuli mjini Molo, wameshuhudia kali ya mwaka baada ya kuwakuta wezi wa mifugo yao wakila nyasi.
Kwa mujibu wa tovuti ya Citizen Tv, tukio hilo lilijiri majira ya saa saba mchana mara baada ya wanakijiji hao kutoka kijiji cha pili walipokwenda kutoa taarifa za wizi huo kwa mganga wa kienyeji.
“Sasa saizi ndio tunatokana kwa “witchdoctor” baada ya sisi wote kuibiwa jana usiku mifugo yetu, ndio tunafika hii Area tunakuta mifugo yetu pembeni huku vijana hawa wakila nyasi” ameeleza shuhuda mmoja ambaye alidai mganga hakutaka apewe pesa mpaka pale mifugo itakapopatikana.