Basi hilo lililokuwa limebeba baadhi ya wachezaji wa tumu hiyo waliokuwa wakitoka mazoezini Uwanja wa Karume, Dar es Salaam lilishambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa mashabiki wenye hasira.
Taifa Stars juzi ilifungwa mabao 3-0 na Misri katika mechi yake ya kwanza ya Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 mjini Alexandria.
Eneo ambalo basi la Taifa Stars limepasuliwa kioo jana |
Wachezaji walikuwa wanatoka mazoezini |
Basi la Taifa Stars likiwa limepaki makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam |
Mabao yote ya Misri yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji Rabia dakika ya 61, Morsi dakika ya 65 na Mohamed Salah dakika ya 70.
Lakini wachezaji ambao walishambuliwa kwa mawe wakiwa kwenye basi hilo, hawakwenda Misri. Kikosi cha Stars kilichokuwa Misri, kinatarajiwa kuwasili leo na kuungana na wenzao waliobaki Dar es Salaam.
Kwa pamoja wachezaji hao watakwenda kambini Zanzibar kwa maandalizi ya mchezo wa CHAN dhidi ya Uganda mwishoni mwa wiki.
Kipigo cha Misri kilikuwa cha nne mfululizo kwa Stars chini ya kocha wake, Mholanzi Mart Nooij baada ya awali kufungwa mechi zote tatu za Kundi B Kombe la COSAFA mwezi uliopita 1-0 na Swaziland, 2-0 na Madagascar na 1-0 na Lesotho mjini Rusternburg Afrika Kusini.
Kwa ujumla huo unakuwa mchezo wa 17 kwa Nooij tangu aanze kuinoa Taifa Stars Aprili mwaka jana akirithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen kati ya hizo akiwa ameshinda mechi tatu tu