Wednesday, June 17, 2015

Urais 2015: Mafuriko Ya LOWASSA Yatua Singida Kwa Kishindo.......Apata Wadhamni 22, 758


Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wea Monduli, Mh. Edward Lowassa, akitoa hotuba ya shukrani kwenye makao makuu ya CCM mkoa wa Singida baada ya kupata wadhamini kufuatia kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
  
Mh. Lowassa ameweka rekodi mpya baada ya kupata wadhamini 22, 758 tangu aanze kutafuta wadhamini mapema mwezi huu
 
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia  wana CCM na wakazi wa Manispaa ya Singida  waklati akiondoka makao makuu ya CCM mkoani Singida Juni 16, 2015 baada ya kupata wadhamini.
 
 
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wana CCM na wakazi wa Manispaa ya Singida wakati akiondoka makao makuu ya CCM mkoani Singida, Juni 16, 2015 baada ya kupata wadhamini.