Wakili huyo ametangaza nia yake hapo jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo tayari alikuwa amekwishakuchukua fomu ya urais aliyoionyesha kwa wananchi.
Alisema aliamua hivyo ili kuijengea nchi misingi imara ya umoja, amani na maadili mema na kupambana na rushwa.
Aliongeza kuwa endapo atateuliwa atahakikisha anapambana na umaskini kuboresha elimu, afya na kumwezesha mtu wa kipato cha chini awe na uhakika wa kuishi katika maisha bora.