Wednesday, June 10, 2015

POLISI ALIYENASWA AKIMNYANYASA BINTI MWEUSI TEXAS AJIUZULU

Ofisa huyo wa polisi akimhenyesha binti wa miaka 15.
Eric Casebolt (41)  akiwa amembana binti huyo.
Video ya tukio hilo iliyowekwa Jumamosi Youtube ikiwa imetazwa na zaidi ya watu milioni 10.

OFISA wa Polisi katika Jimbo la Texas, Marekani, Eric Casebolt (41) aliyenaswa kwenye video akimnyanyasa binti mweusi kwa kumkamata na kumdondosha chini kisha kutoa bastola akiwalenga vijana wengine wawili amejiuzulu. Taarifa zimeeleza kuwa ofisa huyo ameamua kujiuzulu kwa utashi wake mwenyewe jana Jumanne.

Ofisa huyo akiwalenga vijana wawili kwa bastola.
Tukio hilo lililonaswa eneo la McKinney Ijumaa iliyopita linamuonyesha ofisa huyo ambaye ni mzungu akimfunga pingu binti wa miaka 15 baada ya kumdondosha chini bila huruma kisha kuwalenga na bastola yake vijana wengine wawili waliokuwa katika pati eneo hilo. Baada ya tukio hilo, ofisa huyo alisimamishwa kazi.

Waandamanaji wakipinga tukio hilo.
Polisi huyo na wenzake walifika eneo hilo baada ya kuitwa na wenyeji waliokuwa wanalalamikia kuwepo kwa vurugu katika sherehe hizo zilizokuwa zinafanyika kwenye bwawa la kuogelea.
Baada ya tukio hilo kuenea mitandaoni, mamia ya waandamanaji waliandamana kuelekea eneo hilo wakitaka ofisa huyo afukuzwe kazi.