Saturday, June 27, 2015

VIATU VIREFU VYAMUUMBUA KAJALA!

 
Kajala Masanja ‘Kay. Stori: Brighton Masalu
KAJALA Masanja ‘Kay’ amezua miguno na mishangao miongoni mwa wapenzi na wadau wa burudani baada ya kutembea ukumbini bila kuvaa chochote miguuni kufuatia kushindwa kutembea na viatu virefu alivyokuwa amevaa. 


‘Ka-ishu’ hako kalinaswa na‘kijumbe’ wetu hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar,kulikokuwa na sherehe ya harusi ya msanii mwenzake,Haji Adam ‘Baba Haji’.Awali, mwigizaji huyo alionekana mpole na mwenye kutembea kwa ‘machale’ lakini ulipo ka muda wa kuwatuza maharusi, uvumilivu ulimshinda na kuamua kupekua. 
“Mmh! Jamani huyu naye vipi? Au ndiyo kuumbuliwa na viatu? Sasa kutembea pekupeku ukumbi mzima ndiyo nini?,” walisikika akina mama waliokuwa jirani kabisa na mwandishi.Alipoulizwa Kajala kama viatu vimemshinda na kumsababisha avivue, alijibu: “Aah, niache bwana, sitaki kuzungumza chochote kwa sasa,nimechoka mno.