Tuesday, June 9, 2015

WAKENYA Wapagawa na Mwigizaji Rihama Ally..Wampa Kitita Kinono cha Pesa Kucheza Filamu na Tamthilia Nchini Humo

Rihama Ally na Mwigizaji Mwenzake
Msanii mahiri wa filamu nchini Riyama ally amesaini mkataba mkubwa wa kucheza filamu nchini Kenya...kampuni maarufu na wasambazi wa filamu nchini Kenya wamefanya mazungumzo nae mji wa Mombasa na tayari ameshaanza kufanya kazi huku akipewa kitita kinono kwa kushirikiana nao.

Kama hiyo haitoshi wadau wengine wa filamu nchini Kenya wametangaza dau kubwa zaidi ili aweze kucheza tamthilia zinazorushwa kwenye Televisheni mbali mbali nchini humo.

Hii itakua ni habari njema kwa watanzania sasa wasanii wetu tutaweza kuwaona nchi nyingine pia wataweza kuwania tuzo mbali mbali za wasanii kutoja Afrika. Kila la heri Rihama Ally