Alisema sauti hiyo inayomuigiza alitumiwa kupitia simu yake na haikumkwaza zaidi ya kufurahia kwamba watu wengi wanakubali awe bungeni.
- “Nafurahi kwa kuwa wengi wameshanipeleka bungeni wakati mimi ndiyo kwanza nipo katika harakati za kuomba kuchaguliwa kupitia umoja wa wanawake Singida , lakini nafurahia kwa kuwa inaonyesha wengi wananikubali, ila nikipitishwa kuwawakilisha wana Singida bungeni sitaongea kama walivyonirekodi katika sauti hiyo,” alisema Wema kwa furaha.