Monday, June 8, 2015

ZA MWIZI 40! DENTI CHUO KIKUU ANASWA

Kibano! Njemba mmoja almaarufu kwa jina la Babuu amenaswa kisha kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kuvunja na kuiba kompyuta mpakato (laptop) nyumbani kwa mtu, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda kamili.
Mwizi maarufu alifahamika kwa jina la babuu pichani akiwa amewekwa chini ya ulinzi na raia wenye hasira kali.
Tukio hilo la kinyama lililoshuhudiwa na Makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers lilijiri wikiendi iliyopita, majira ya saa 8:00 mchana kweupe, maeneo ya Mwenge jijini Dar ambapo OFM, wakiwa ‘wanarandaranda’ kusaka matukio, walisikia sauti za ‘mwiziii...mwiziii...mwiziii..’ na kushuhudia umati ukimuangushia kipigo mtu huyo waliyedai aliiba laptop hiyo kwenye nyumba moja iliyopo eneo hilo.
Babuu pichani akitoa maelezo baada ya kupewa kichapo na raia kwa madai ya kuiba laptop aina ya Apple.
Katika utetezi wake, jamaa huyo alidai yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja maarufu jijini Dar (jina tunalo) na kudai kuwa laptop hiyo aliichukua kwa mtu ambaye anamdai aliyemtaja kwa jina moja la Ford.
Wananchi hao waliokuwa wakimsulubu walikuwa wakipingana wengine wakidai kuwa madai ya mtu huyo yanapaswa yachunguzwe kwanza kabla ya kupigwa, huku wengine wakitaka auawe kwani alikiri kuchukua laptop isiyo yake.
Mwizi huyo akiwa nje ya chumba alichofanyia uhalifu na kuonyesha baadhi ya vifaa alivyoiba.
Raia wakimhoji babuu baada ya kumkamata na laptop.
Mwizi huyo akiendelea kupokea kichapo.
Hata hivyo, watu hao walikubaliana kumpeleka mtuhumiwa huyo hadi kwenye nyumba anayodaiwa kuvunja na kwenda naye ‘msobemsobe’ ambapo watu walishuhudia mlango wa chumba cha mtu ambaye hakuwepo muda huo, ukiwa wazi na kitasa kikiwa chini ukiashiria kuvunjwa.
Kama hiyo haitoshi, Babuu, katika harakati za kukurupuka eneo hilo aliacha begi lenye laptop tatu ambapo moja alikiri kuichukua kutoka ndani ya chumba hicho.
Mbali na laptop hizo, njemba huyo alikutwa na bisibisi na funguo zaidi ya 18 za vitasa tofauti huku funguo moja ikitajwa kama ‘funguo malaya’ ambayo hufungua kitasa chochote.
Baada ya kumnasa na funguo hizo, wananchi hao walimvua nguo na kumuacha akiwa na ya ndani pekee huku baadhi yao wakiomba wamfanyie ‘kitu mbaya’ lakini machozi yake na kuloa damu chapachapa vikamuokoa.
Kama upepo taarifa zilifika kwa mwenye chumba ambaye alifika na kudai kuwa hamfahamu mtu huyo ndipo kipigo cha kufa mtu kikaendelea huku umati ukiruka ukuta wakitaka kutoa adhabu kila mmoja kwa mtindo wake.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Chacha alifika eneo la tukio na kukiri kupata malalamiko ya mara kwa mara ya wizi wa majumbani kutoka kwenye nyumba hiyo ambapo wizi huwa ni wa mashuka na nguo ambazo huanuliwa zikiwa zimeanikwa.
Mwenyekiti huyo alitumia busara kuwazuia watu wasimpige jamaa huyo kisha kuwataarifu polisi waliofika eneo la tukio na kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi na matibabu.