Katika kipindi cha Asubuhi cha cha jana ITV alialikwa Askofu wa kanisa Katoliki ambaye alinishangaza kwa jambo jipya.
Alisema wala tusishangae yanayo fanywa na serikali ya CCM ni matokeo ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa mashehe fulani wa Bagamoyo ambao walifanya tambiko ili Nchi ipate uhuru chini ya mwalimu Nyerere kwa kibali cha mizimu.
Kusema ukweli hata mimi niliwahi kumsikia Mwalimu akisema hao wazee walimwambia aruke shimo moja lililo fanyizwa dawa kisha akaambiwa mkoloni hakuwezi.
Sasa kwa mjibu wa mtumishi huyo wa Mungu anasema hata Uhuru ulipo patikana nchi ili kuwa chini ya laana kubwa kiasi kila jitihada zilikuwa zikienda mrama daima.
Yeye ansema ameoteshwa juzi tu kuhusu mkasa huo na kuambiwa Watanzania wasipotubu tuta kuwa tuna shuhudia viongozi wetu wakifanya vituko.
Aliongeza kuwa tabia ya mtu aliye laaniwa inajulikana anakuwa haelewi anafanya nini.Mkimlaumu atakuwa ana washangaa ninyi.
Anasema madudu yote ya CCM mathalani kutoa nguzo za umeme toka mafinga kupelekaKenya na kisha kurudisha Nchini kwa kununua kwa fedha za kigeni ni jambo linalo weza kufanywa na waliolaaniwa tu.
Chanzo: ITV