Wednesday, July 15, 2015

DAH WEMA SEPETU NA ANTI EZEKIEL WAINGIA KATIKA BIFU JIPYA KABISA KISA HIKI HAPA

filamu Bongo, ambao walikuwa mashosti kwa
muda mrefu kabla ya kidudumtu kuingilia kati
hivi karibuni na kusuluhishwa, hivi sasa bifu
kati yao limeanza upya, Risasi Mchanganyiko
linakujuza.
Chanzo chetu ambacho hakipepesi macho
kinasema tangu Aunt ajifungue mtoto, Wema
hakuwahi kukanyaga nyumbani kwake kwa ajili
ya kumuona, kutoa hongera au hata pole kwa
rafiki yake huyo, isipokuwa wamekuwa
wakichati kupitia simu za mikononi, kitu
ambacho si sahihi.
Lakini kali zaidi, ni kitendo cha Wema
kushindwa kuhudhuria sherehe ya kutimiza
siku 40 tangu azaliwe mtoto huyo, Cookie, kitu
kilichomfanya mwenzake kumuondoa kabisa
katika orodha ya marafiki zake.
“Yaani Aunt kipindi chote alimvumilia akijua
huenda yuko ‘bize’, lakini kwa kutofika kwenye
siku hiyo muhimu, amemtoa kabisa akilini
mwake,” kilisema.
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili
lilimtafuta kwa njia ya simu Aunt ili kuthibitisha
ubuyu huo, lakini akakubali tu juu ya
kutohudhuria kwenye tukio hilo muhimu la
mtoto wake, licha ya kuwa alimpa taarifa.
“Hakuja, lakini siwezi mlaumu sana, labda
alikuwa na majukumu mengi, ukizingatia hivi
sasa ana mambo ya ubunge,” alisema.