Friday, July 3, 2015

DIAMOND AKIRI KUMPENDA OMOTOLA

KING wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametengeneza kichwa cha habari nchini Nigeria baada ya kufunguka kuwa anampenda ‘vibaya’ staa wa filamu nchini humo, Omotola Jalade Ekeinde, Ijumaa lina stori kamili.
King wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond katika ziara ya kimuziki iitwayo ‘Nana Tour’ nchini humo, staa huyo ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mjasiamali maarufu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amekuwa akiumizwa na penzi la Omotola kitambo sana lakini hakuwahi kuzungumza katika vyombo vya habari.
OMOTOLA_NdaniTV_Daniel-Sync-PHOTOS-13-Edited-1Staa wa Nollywood nchini Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde ‘Omotola’.
“Diamond ana maumbo yake flani hivi amazing ambayo huwa anayapenda, siku nyingi sana kabla hata hajakutana na Zari, alikuwa akituambia watu wake wa karibu kwamba miongoni mwa wanawake mastaa ambao anawatamani awaweke kwenye himaya ya penzi lake ni Omotola.
“Alisema anampenda kwa kila kitu kuanzia ufanyaji kazi wake, umbo lake na hata umaarufu mkubwa alionao ndani na nje ya Bara la Afrika,” kilisema chanzo hicho.
Omotola-Jalade-Ekeinde-on-CNN-African-Voices-January-2014-BellaNaija-021Baada ya chanzo hicho kueleza habari hiyo, mapema wiki hii, mtandao wa nigeriafilms.com ulithibitisha maneno hayo kwa kuposti habari iliyobainisha Diamond anampenda Omotola sanjari na mastaa wengine wawili wa Nigeria anaovutiwa nao kimapenzi.
Akiwa hewani alipokuwa akihojiwa na redio moja jijini Lagos, Diamond aliweka bayana kuwa anateswa na penzi la mastaa watatu Nigeria, Omotola, Tonto Dikeh na Genevieve Nnaji.
“Jamaa kitambo sana anateswa na penzi la Omotola sasa leo kaongeza na wengine wawili na ninavyomjua hashindwi kufanya kweli ingawa nina wasiwasi kwa Omotola na Tonto maana wana waume zao labda ajiweke kwa Genevieve ambaye hajaolewa,” kilikazia chanzo chetu.Diamond hakupatikana ili kusikia kauli yake juu ya ishu hiyo.