Na Gladness Mallya
BAADA ya hivi karibuni kutangaza nia ya kugombea ubunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) huko Morogoro Vijijini alikozaliwa, staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma ameibuka na kueleza kwamba ameamua kufanya hivyo ili kuwatetea walemavu na watoto wa kike.
Akipiga stori na Ijumaa, Wastara alisema wananchi ambao ni walemavu wamekuwa hawatendewi haki katika maeneo mbalimbali kulingana na maumbile yao hivyo lengo lake kubwa ni kwenda kutetea haki zao ili ziwe sawa na watu wengine pamoja na sanaa kwani wasanii wamekuwa wakinyonywa kutokana na kazi zao kuuzwa hovyo.
Naamini nitashinda, kwani jimbo nililochagua mimi ni mzaliwa na nimekuwa mwakilishi wa akina mama na watoto kwa muda mrefu. Sasa ni wakati wa kwenda kuwawakilisha huko bungeni, alisema Wastara.