Friday, July 3, 2015

NISHA: KISIASA BADO NIPONIPO, NAENDA ZANGU CHINA KUTOA VICHEKESHO

IMG-20150630-WA0001Staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ akipozi.
Na Hamida Hassan
Staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa hatarajii kugombea wala kujiingiza kwenye siasa kwa sababu bado yupoyupo katika eneo hilo.
niishaa baada ya mekapAkizungumza na Ijumaa, Nisha alisema kuwa, katika kipindi hiki cha mikikimikiki ya siasa atakuwa nje ya nchi kwani anatarajia kwenda China mwezi huu alikoitwa kufanya vichekesho.
“Nimepata dili, nitakwenda China kwa ajili ya kufanya comedy (vichekesho), nimepata fursa lazima niitumie ipasavyo. Kuweka muvi zangu mtandaoni kumenisaidia sana hivyo kwenye mambo ya siasa bado niponipo sana,” alisema Nisha.