SIKU chache baada ya nyota wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila, ‘Ray C’ kutangaza anatafuta mchumba, kijana aliyejitambulisha kwa jina la Abubakar Ally ‘Babuu’ (21) amejitokeza akisema yeye anataka ndoa na Ray C.
….Akigonga geti nyumbani kwa Ray C.
Babuu alinaswa na mapaparazi wetu hivi karibuni Hospitali ya Mwananyamala, Dar Kitengo cha Waathirika wa Madawa ya Kulevya (Methadone) ambapo Ray C hufika kila siku kwa ajili ya dozi.
Ni baada ya kutonywa na vyanzo, mapaparazi wetu walifika eneo hilo na kumshuhudia kijana huyo akizuiwa kuingia hospitalini hapo na mlinzi.
…Akielekea ofisini kwa Ray C.
Mapaparazi wetu walifanikiwa kuzungumza naye ambapo alikiri kumsaka Ray C kufuatia tangazo lake kwenye mtandao wake wa Instagram kwamba anatafuta mwanaume wa kumuoa.
Babuu aliwaomba mapaparazi wetu wamuelekeze nyumbani kwa Ray C baada ya kumkosa kwenye Jengo la Biashara Complex, Mwananyamala.
Babuu aliwaomba mapaparazi wetu wamuelekeze nyumbani kwa Ray C baada ya kumkosa kwenye Jengo la Biashara Complex, Mwananyamala.
“Mimi nataka kumuoa Ray C. Amesema kwenye tangazo lake Instagaram kwamba, mwanaume anayemtaka awe tayari kushea naye simu. Niko tayari, tena nitampa mapenzi yangu yote, nisaidieni kunielekeza kwake,” alisema Babuu.
Akaendelea: Nataka nimuoe. Mambo ya umri na pesa si vitu vya kuviangalia kwenye mapenzi.”
….Akigonga mlango wa ofisi ya Ray C.
Ilibidi mapaparazi wetu waongozane na kijana huyo hadi nyumbani kwa mwanadada huyo, Bunju, Dar
huku akiwa na mfuko mweupe ambao alidai ndani yake mlikuwa na barua ya posa na zawadi ya kadi.
Babuu aligonga geti kubwa, msichana mmoja alitoka na kujitambulisha kuwa ni ndugu wa Ray C. Alisema Ray C hakuwepo ndani ya nyumba hiyo.
“Bado sijakata tamaa, nitamtafuta kila mahali hadi nimpate. Najua siyo rahisi, nimemtumia meseji na kumpigia simu lakini hapokei,” alisema Babuu.
Ray C alipotafutwa na Amani juzi kutaka kujua kama anafahamu alitafutwa alisema: “Siyo huyo tu. Wamenitafuta wengi sana. sikujua kama ishu itakuwa kubwa hivyo… Teh! Teh! Teh!”