Huyu hapa ni mhe.Jerry Silaa alikuwa na haya ya kusema.....
Namshukuru Mungu nimerudisha fomu salama.....
Nawaomba wanaCCM waniunge mkono kwenye mchakato huu...
Kuanzia 22/7/2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi itafanya zoezi la kuboresha Daftari la wapiga kura kwa mfumo wa BVR mkoani DSM. Natoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.
Eid Mubarak..
Hili ni ombi maalum kwa wananchi wa Ukonga toka kwa meya huyo mstaafu wa manispaa ya Ilala Mhe.Jerry Silaa wakati akijiandaa kurudisha form hizo za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kupitia CCM kwa jimbo la UkongaZifuatazo ni picha Mbalimbali zilizopigwa na Mpiga Picha Fred Chegge kwa niaba ya Jerry Silaa Foundation katika tukio hilo la urudishaji form hizo lilolofanyika leo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala.
Masama Blog inamtakia kila la kheri katika Hatua hii ya kuomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa jimbo la ukonga kwani tunaamini ameonyesha uwezo mkubwa wa uongozi katika kipindi alichoweza kuwa meya wa manispaa wa ilala.