Friday, July 17, 2015

Msanii Ester Kiama Amwaga Machozi baada ya Kudaiwa ana UKIMWI


Msanii anayekuja kwa kasi katika anga la filamu, Ester Kiama amejikuta akiangua kilio kufuatia madai yanayoenezwa kuwa ana ‘ngoma’. 
 
Taarifa ya ‘kuungua’ kwa staa huyo zimekuwa zikisambaa kama moto wa kifuu kwenye mitandao ya kijamii huku mwenyewe akidai anasingiziwa na hivyo juzi kati akaamua kwenda kupima.
 
“Hizi habari kwamba nina ngoma zimekuwa zikienea sana na hakuna kitu kibaya kama kumnyooshea mwenzako kidole bila kuwa na uhakika na unachokisema. Nakumbuka mara ya kwanza kuna mwanamke aliandika mtandaoni kuwa nimeathirika hivyo Dude ajihadhari.
 
“Niliumia sana lakini ili kuwakomoa nikaenda kupima na majibu yakaonesha niko safi, nikajikuta nalia sana, si unajua inavyouma kusingizwa kitu? Sasa ili kuwakata kilimilimi hao wanaonizushia, majibu haya nitayabandika mtandaoni pia,” alisema Ester.