Friday, July 17, 2015

WAREMBO WAZICHAPA KUGOMBEA BWANA

SAMSUNG CAMERA PICTURESWarembo hao wakitoana jasho mbele ya kadamnasi.
Saimeni Mgalula, Mbeya
NI kioja kilioje! Hata kuku siku hizi inadaiwa waliacha kuzichapa! Lakini wadada wawili ambao wote wanauza pombe kwenye glosari tofauti na majina yao hayakupatikana kabisa, wamejikuta wakiwatazamisha watu sinema ya bure kufuatia kuzichapa hadharani tena mchana wa mwezi mtukufu.
SAMSUNG CAMERA PICTURES…Wakizidi kupeana shughuli.
Tukio hilo liliibuka Julai 13, mwaka huu saa 5 asubuhi katika maeneo ya Makontenani Kata ya Makambini wilayani Momba, mkoani hapa.
Akizungumza na paparazi wetu, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema:
“Sisi tulianza kusikia wakitukanana matusi huku wakisogeleana. Lakini hatujui chanzo ni nini!”
Hata hivyo, shuhuda aliyejitambulisha kwa jina moja la Hassan alisema kwa maneno waliyokuwa wakiyazungumza katika kurushiana matusi warembo hao, sababu ni kugombea mwanaume.
SAMSUNG CAMERA PICTURES…Wakiamuliwa.
Inadaiwa kuwa, kurushiana matusi kulipopitiliza heshima, kila mmoja alitoka nje ya glosari yake na kushikana kisha kuanza kuzichapa hali iliyosababisha kujaza watu na kufunga barabara.Shuhuda mwingine ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alisema kuwa ni halali yao kupigana kutokana na eneo hilo kuwa na sifa ya wasichana kuibiana mabwana.
SAMSUNG CAMERA PICTURESKwa upande wao, mashuhuda wengine ambao walikuwepo walilaani kitendo hicho kwa kusema kuwa si maadili mema kwa kizazi cha sasa ambacho kilikuwa kikishuhudia mpambano huo haramu.
“Sisi wakazi wa eneo hili hatupendi vurugu za watu kupigana tena hadi kuvuana nguo hivi. Wanaifundisha nini jamii? Hawa wangekuwa nchi nyingine wangeshitakiwa kwa kupigana hadharani na kutoleana matusi ya chumbani,” alisema mzee mmoja.
Mpaka paparazi wetu anatoweka eneo hilo,  wasamaria wema walikuwa wakiendelea na jukumu la kuwaachanisha.