Wednesday, August 12, 2015

Doctor wa Chelsea bado mambo hayaeleweki, mengine ni haya baada ya kusimamishwa..

Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho bado anaamini kuwa mkuu wa madaktari wa timu hiyo Eva Carneiro alifanya uzembe wakati wa kumtibia Eden Hazard kitu kilichopelekea Mourinho kuona kama anachelewesha muda wakati mchezo ulikuwa katika dakika za nyongeza.
evapa_3222081b
Taarifa zilizotoka August 11 kuhusiana na Doctor huyo huenda hatasafiri na timu wiki ijayo katika mechi dhidi ya Mancherster CityEva Carneiro bado ataendelea kuwa mkuu wa madktari wa timu hiyo ila hatoruhusiwa kwenda katika mazoezi ya timu hiyo na hata wakiwa katika Hotel kitu ambacho kimezua maswali mengi juu ya hatma ya Doctor huyo katika timu hiyo.
BvwYuz8IMAA8q4d
Baada ya Mourinho kumlaumu Eva  baadhi ya watu katika mitandao mbalimbali ya kijamii walimpongeza Eva kwa maamuzi aliyoyafanya na wao wanaamini alikuwa anatekeleza majukumu yake kama Doctor wa timu hiyo.