Ulimwengu una maajabu mengi na mitandao ya
kijamii inatusaidia kuyafahamu. Uhusiano wa
Diamond na Zari the Bosslady haujawahi
kupokelewa vizuri na ex wake Ivan aliyezaa naye
watoto watatu wa kiume.
Watoto hao wameendelea kuwa karibu na wazazi
wote wawili. Uhusiano wa ulipoanza tu, Ivan
kupitia mpambe na rafiki yake wa karibu, King
Lawrenc walianzisha vita kwenye mitandao ya
kijamii kuwashambulia Diamond na Zari. Hakuna
shaka kuwa Ivan amekuwa akionesha hisia zake za
kutoupenda uhusiano wao kupitia Lawrenc ambaye
amekuwa akiwashambulia mfululizo.
Katika kipindi ambacho tension kati ya Diamond na
Alikiba zimefika kileleni hususan kipindi cha
kuelekea tuzo za KTMA 2015, Ivan mwenyewe pia
alishiriki katika kampeni za kumuombea kura
Alikiba. Ni wazi kuwa Ivan bado hajakubali yaishe,
na kumuona mke wake wa zamani akiwa na furaha
na Diamond ni kitu kinachomkera zaidi.
Na sasa wakati uhusiano wa Diamond na Zari upo
katika kilele cha furaha baada ya kujaaliwa mtoto
wa kike, Latiffah, kambi ya Ivan kupitia mpambe
wake Lawrenc imedhamiria kuitilia doa furaha hiyo.
King Lawrenc ameanza kutupa mashambulizi kwa
Diamond na kueleza kile anachoamini kuwa Tiffah
ni mtoto wa Ivan! Kwa historia ya kile Lawrenc
amekuwa akikisema tangu mastaa hao waanzishe
uhusiano, ni wachache wanaoweza kuamini
‘upuuzi’ huu lakini kiukweli hiki ni kitu
kinachoweza kuwakosesha raha Diamond na Zari,
kama wakiamua kumjali.
Lawrenc alianza kupost picha ya mtoto mchanga
na picha ya Ivan na kuandika, “No DNA Needed.
The best revenge has shown itself after 9months.
Anamaanisha kuwa mtoto huyo ni Tiffah na
kwamba Ivan ndio baba yake.
Hadi sasa hakuna picha iliyotolewa inayoonesha
sura halisi ya Tiffah hivyo ni ujinga kuamini kuwa
aliyoweka Lawrenc ni yake. Na katika yote
yanayoondolea, Zari na Diamond hawawezi
kuruhusu picha ya mtoto wao ifike kwenye mikono
ya adui yao labda kama wao wenyewe wakiamua
kuipost kwenye mitandao ya kijamii, kitu ambacho
bado hawajakifanya hadi sasa.
Na pengine mambo kama haya ndio yanamfanya
mama mzazi asite kuionesha sura ya binti yake
huyo. “I swear I wanted to show you her face but
she turned away saying, nope i want no drama.
She knows y’all can be dramatic. She’d rather
stay safe for now… too many judges, advisors,
teachers you name it you’ll find it on IG. I bet she
can’t deal,” aliandika Zari.