Wem Sepetu ‘Madam’ akidendeka na mwanaume mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli iliyopo Msasani jijini Dar.
Mwandishi wetu
Licha ya kudai kwamba skendo za ngono sasa basi, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekwaa aibu mpya baada ya picha zake kunaswa akiwa na mwanaume mwingine kwa mara nyingine, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli iliyotajwa kwa jina la Cape-town Fish Market iliyopo Msasani jijini Dar.
MADAI MAZITO
Chanzo chetu ambacho ni makini kilipenyeza kuwa, katika tukio hilo la hivi karibuni, staa huyo alikuwa hafahamiani na mwanaume huyo, lakini kuna kijana mmoja ambaye mara nyingi anawakuwadia mastaa wa Bongo kwa matajiri, alidaiwa kumtonya Wema kuwa kuna ‘mchati’ anataka kutoka naye.
Kilifunguka kwamba, baada ya Wema kung’atwa sikio juu ya Mkongomani ambaye ana ‘hela chafu’, alidaiwa kuonekana kuchachawa hivyo eti alikubali kupelekwa kwake akajazwe ‘mihela’.