MWANADADA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kusema hawezi kumrudia aliyekuwa mpenzi wake, msanii Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Salma Jabu ‘Nisha’.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, Nisha alisema amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa ana mpango wa kurudiana naye, jambo alilosema haliwezekani kwani kwake hana tabia ya kula matapishi.
“Siwezi kurudiana na Nay, kwanza ana mwanamke mwingine na kuzaa naye japo wameachana, mwanzo nilimuogopa sana nikimuona, lakini hivi sasa nimeshamzoea, tumebaki kama kaka na dada, suala la mapenzi haliwezi kujirudia tena,” alisema.