Tayari mpaka sasa tumeona Mastaa mbalimbali wa Tanzania ambao hawajaficha hisia zao ni nani wanamkubali zaidi kwenye kumpa uongozi wa nchi na nafasi nyingine zinazogombaniwa.
Pamoja na kwamba Ali Kiba ameonekana kwenye headlines za kampeni za CCM, hakuwahi kuandika au kupost chochote kwenye kurasa zake kuhusu kiongozi gani anaeona ni sahihi kwake ila sasa ndio amefanya maamuzi hayo kwa mara ya kwanza.
Ali Kiba aliandika kwenye page yake ya Instagram >>> ‘Chaguo langu sahihi MAGUFULI#hapakazitu #KingKiba‘ na kisha Kiba baadae akaweka picha nyingine ya Dr. Magufuli na kuandika ‘ MAGUFULI #hapakazitu #KingKiba‘