Siku ya kupatikana kwake, umati ulijitokeza kumshuhudia mpotevu huyo alipokutwa kichakani karibu na mtu huyo aliyedaiwa kumchezea uchawi.
….Akiwa kichakani alikofichwa.
Akizungumza baada ya kupatikana, Christine alisema kuwa, siku ya tukio alikuwa amelala nyumbani kwake kijijini hapo ambapo watu wawili (mmoja aliyekamatwa na polisi) waliingia chumbani na kumchukua.Alisema baada ya kuchukuliwa alijikuta kwenye kundi la watu ambao baadhi yao aliwatambua kwa sura na majina na walifariki dunia miaka mingi.
“Wale watu wanatumikishwa kazi ngumu na kulishwa chakula kibovu katika maeneo ambayo ni karibu na ziwa.
“Miongoni mwa hao watu nilimtambua marehemu baba mkwe wangu na dada mmoja aliyekuwa akishona kwa cherehani. Mimi nilipofika nilianza kupigwa na kuamrishwa kulima na kula chakula kibovu lakini nilikataa,” alisema Christine.
Mume wa mwanamke huyo, Itembe Mwikwabe alisema baada ya mkewe kupotea katika mazingira tata alikwenda polisi na kukandikiwa jalada loenye namba TURG/RB/14/2016 TAARIFA.Alisema baada ya kutofanikiwa kumwona mkewe aliamua kwenda kwa mganga wa kienyeji ambaye ndiye aliyefanikisha kupatikana kwa mkewe.
“Sasa ninamchukua mke wangu na kumpeleka akatibiwe kwani namwona hana akili timamu,” alisema Mwikwabe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kitenga, Yohana Nyangi alisema baada ya kupata taarifa ya kupotea kwa mwanamke huyo ofisi yake ilimpa barua mumewe aende polisi.
“Tukio hili linapaswa kulaaniwa, lakini ninaonya mtu yeyote asihusike kutenda jinai juu ya hawa wanaotajwa kuhusika na mazingira haya wala familia yake na mali zake kwani tayari Agness ameshakamatwa na polisi.”