Sunday, September 27, 2015

MESSI KUKAA NJE YA UWANJA KWA MUDA WA WIKI NANE BAADA YA KUPATA MAJERAHA KWENYE MECHI YA LIGI YA SPAIN HAPO JANA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi ameingia katika headlines baada ya kushindwa kuendelea na mechi dhidi ya Las PalmasLionel Messi alilazimika kufanyiwa mabadiliko baada ya kuumia goti.
fd1754d8-9fe5-4ab2-b027-eb23a810d149-2060x1236
Lionel Messi alitoka nje kupatiwa huduma na kurudi uwanjani ila alishindwa kuendelea na mchezo, hivyo kocha wa FC Barcelona Luis Enrique alilazimika kufanya mabadiliko na kumuingiza Munir El Haddadi dakika ya 10 ya mchezo na Lionel Messi kwenda benchi. Lionel Messi alipata jeraha hilo baada ya kuchomekewa mguu na beki wa Las Palmas Pedro Bigas Rigo.
2CC9889400000578-0-image-a-8_1443278181067
Mitandao mingi barani Ulaya imethibitisha Lionel Messi kuwa atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nane ambapo ni sawa na muda wa miezi miwili. Licha yaLionel Messi kutolewa nje mapema, mechi hiyo ilimalizika kwa klabu ya FC Barcelonakuibuka na ushindi wa goli 2-1 magoli ambayo yalifungwa na Luis Suarez,  Jonathan Viera akiipatia Las Palmas goli la kufutia machozi dakika ya 88.
Video ya tukio la Messi