Monday, September 21, 2015

Mh.Lowassa ameingia mkoani Mtwara kwa kishindo na kupokelewa na maelfu ya watu.



Mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema huku akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh Edward Lowassa ameingia mkoani Mtwara kwa kishindo na kupokelewa na maelfu ya wakazi wa mkoa huo.
Jumatatu tulivu ya sept 21, mji wa Mtwara na viunga vyake vyote ulizizima ambapo shughuli nyingi tu zikisitishwa huku wao nao wakiamini kuelekea Oct 25, sauti bado ni moja tu.

Akihutubia maelfu ya wakazi wa Mtwara Mh.Edward Lowassa amewahakikishia kuwa serikali yake ya awamu ya tano itajikita katika kuimarisha uchumi ikiwa ni pamoja na kuwafanya wakazi wa mji wa Mtwara kunufaika kikamilifu na rasilimali za gesi na mafuta huku akiwahakikishia pia upatikanaji wa soko la uhakika la mazao ya Korosho.
Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu, amewataka wakazi wa Mtwara kuhakikisha wanamchagua kwa kura nyingi Edward Lowassa kwani kushindwa kufanya hivyo ni kuifanya Mtwara na mikoa ya kusini kwa ujumla kuzidi kuwa nyuma kimaendeleo.

Kutokana idadi kubwa ya maelfu wanaozidi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Edward Lowasa, viongozi wa ngazi ya juu wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, wanaamini ni dhahili mabadiliko ya Oct 25 hayakwepeki.
Akiwa mkoani Mtwara na timu yake ya kampeni Edward Lowassa alifanikiwa kuhutubia mikutano mikubwa ya hadhala katika majimbo ya Tandahimba, Newala kabla ya kuhitimisha katika uwanja wa mashujaa ambapo hata hivyo uwanja huo ulijikuta ukishindwa kuhimili kishindo cha mgombea huyo wa nafasi ya urais.