Mwenyekiti wa Chama cha DP,Mchungaji Christopher Mtikila ,leo asubuhi alikuwa Live Star Tv katika kipindi cha Tuongee Asubuhi ambapo ameongelea mambo mbalimbali kama;
- Dhana ya ufisadi na aina za viongozi tunaohitaji kuwapatia Ikulu
- Umuhimu wa afya bora kwa wagombea uraisi
- Ahadi za CCM na CHADEMA Kutoa elimu ya bure
- Mapungufu Ya Edward Lowassa.
- Tafiti zilizofanywa na SYNOVATE pamoja na TWAWEZA juu ya nani ana nafasi ya kushinda uraisi
Hapo chini kuna video za maongezi yake ambazo utapata nafasi ya kuzisikiliza, lakini kabla ya video hizo, haya ni baadhi ya mambo aliyoyaongea Mtikila.
1-Sababu iliyofanya ngombea mwenza wake kutotokea ni dharura ya ugonjwa iliyompata mkewe huko Zanzibar na amesema Jumaatatu yake alienda ofisi za tume kufuatilia akaambiwa mwenyekiti Jaji Lubuva hajafika ofisini anaumwa hivyo akawaambia naye jaji Lubuva kwa kushindwa kuhudhuria ofisini kwa sababu ileile naye akatwe.
Amesema amepeleka kesi mahakama kuu na wiki ijayo ndio inatolewa uamuzi.
Amesema amepeleka kesi mahakama kuu na wiki ijayo ndio inatolewa uamuzi.
2. Mtikila amesema kafungua mashtaka kuzuia Lowasa kuendelea kugombea urais kwa hoja ya afya yake akijenga hoja kwamba muajiriwa yoyote lazima apime afya yake hivyo lowasa anakosa sifa hiyo ya kupewa nchi.
3. Amesema watanzania tunaumwa epidomia, mwenyewe kauita niunyani, yaani tukipewa kanga kofia viroba tunashabikia tu.
4. Amesema wanachama na viongozi wa chadema bangi na gongo kwao ni kama sakrament.
5.Amesema Lowasa ni tapeli kwa kuwa alitudanganya anaenda kutununulia mvua.
6. Alipoulizwa nani anamuona anaweza kuibadili Tanzania kati ya Lowasa na Magufuli alijibu magufuli ndio sahihi japo ana mapungufu yake lkn zaidi yake yeye ndio anafaa.
Video ya kwanza: Mchungaji Christopher Mtikila akinadi sera za chama chake
Hapo chini kuna Video za Maongezi Yake
Video ya kwanza: Mchungaji Christopher Mtikila akinadi sera za chama chake
Video ya Pili: Mchungaji Christopher Mtikila akizungumzia tafiti zilizofanywa na SYNOVATE pamoja na TWAWEZA juu ya nani ana nafasi ya kushinda uraisi katika uchaguzi mkuu.
Video ya Tatu: Mchungaji Christopher Mtikila akimkataa Lowassa kwa madai kuwa ana mapungufu mengi yaliyowazi hivyo hamuungi mkono.
Video ya Nne:Mchungaji Mtikila awachambua wagombea uraisi wa CCM na Chadema na ahadi zao za kutoa elimu bure kama vipaumbele vyao.
Video ya 5: Mchungaji Mtikila Azungumzia Afya kwa Mgombea Uraisi
Video ya 6:Mwenyekiti wa DP Mchungaji Christopher Mtikila akizungumzia dhana ya ufisadi na aina za viongozi tunaohitaji kuwapatia Ikulu.