Post hii inamilikiwa na msanii wa bongofleva Nay wa Mitego ambaye alitangaza toka mwanzoni kwamba anamuunga mkono mgombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu wa October 25 2015.
Nay amekua akipost vitu mbalimbali kuhusu siasa za Tanzania lakini leo September 23 amepost kwa kuandika >>> ‘Wasanii tubaki kuwa wahamasishaji tu kuanza kukashfu viongozi utadhani labda nawewe umekua mwanasiasa au Mgombea itakuja kutu Cost baadae’
‘Huwa najiuliza cjui wanalipwa shiling ngapi maana wanasahau wao ni wasanii na wana mashabiki wenye Imani tofauti, pia kuna Maisha baada ya uchaguzi, endeleeni kutumika vibaya kwa njaa ya leo na kwa maslahi ya wachache na kusahau kuna kesho,Pigania unacho amini lakini sio kwa kashfa wala Matusi, Mimi naamini #Mabadiliko2015 Tukutane #October25′ – Nay wa Mitego