Thursday, October 8, 2015

Kingunge Kumnadi Lowassa Leo Arusha..Aomba Dakika 40 za Kumchana Chana Kikwete na CCM

Aliyekuwa kada mkongwe wa CCM mwenye kadi namba 7, ameomba muda wa dakika 40 za kumchana chana raisi Kikwete kwenye mkutano wa kampeni utakaofanyika leo jijini Arusha. 


Mwanasiasa mkongwe na mmoja kati ya waasisi wa Tanu na CCM aliyetangaza kuachana na chama hicho hivi karibuni, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amepanga kupanda rasmi kwenye jukwaa la Ukawa, leo jijini Arusha kumnadi mgombea wa Chadema, Edward Lowassa.
 
Taarifa za Kingunge kumnadi rasmi Lowassa leo, zimethibitishwa na meneja wa kampeni wa Chadema, John Mrema.
 
“Kesho (Leo) Kingunge atangumza na watanzania kueleza kile anachokiamini, anataka mabadiliko, cha muhimu ni ujumbe wake,” Mrema alikaririwa  jana

Mzee  Kingunge  alitangaza  kuachana  na  CCM  kwa   madai  kuwa  chama  hicho  kimepoteza  mwelekeo.
  
Alisema  utaratibu  uliotumiwa  kumpata  mgombea  Urais  wa  chama  hicho  kupitia  vikao  vya  kamati  ya  maadaili  na  usalama  vilienda  kinyume  na  taratibu  na  katiba  ya  chama  hicho  kwa  maslahi  ya  viongozi  wachache.


Mwanasiasa  huyo  mkongwe  alisema  hatajiunga  na  chama  chochote  cha siasa  kwa  sasa  lakini  atabaki  kuwa  upande  wa  wale  wanaotaka  mabadiliko  ya  kuiondoa  madarakani  serikali  ya  CCM