STAA wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema ana mpango wa kuchora tena jina la mpenzi wake, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kwenye moja ya kalio lake ikiwa ni njia mojawapo ya kuonyesha mapenzi yake ya dhati kwake.
“Mimi bado tatoo moja ya muhimu sana ambayo nataka kuchora kwenye kalio ili kuonyesha ni jinsi gani nampenda mpenzi wangu Nuh,” alisema Shilole.