MASKINI! Mume wa mwigizaji wa Bongo Movies, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’, Gadner Dibibi amewataka watu wanaomsema mkewe huyo kuwa hapati mtoto, waache kwani wanajisumbua bure suala hilo ni la Mwenyezi Mungu.
Akizungumza na gazeti hili, Dibibi alisema alipomuoa Jack siyo kwamba alikuwa akifi kiria mtoto ila alijua mtoto analetwa na Mungu hivyo anaamini kuwa watampata tu hivyo amezidisha kumpenda.
“Mtoto ni majaliwa jamani, nilimuoa na nilijua wazi ipo siku Mungu akibariki tutapata mtoto na hata tukikaa miaka kumi bila mtoto siwezi kumuacha mke wangu kwa sababu hiyo, nampenda na nitaendelea kumpenda,” alisema Dibibi.