Mashimo ya kupenya ndani kwa ndani chini ya ardhi yamevumbuliwa kwenye machimbo ya chokaa Kaskazini mwa Ufarasa na yanasadikika kuwa wanajeshi wa Uingereza waliishi humo wakati wa mapigano ya Vita vya Kwanza vya Dunia (WW1) vilivyofanyika kati ya waka 1914 hadi 1918.
Ndani ya mashimo hayo kumekutwa miamba migumu ambayo imeandikwa majina ya wapiganaji wa WW1 waliokufa na kuzikwa mule. Pia kuna makanisa ambamo waliabudu, mabaki ya gari na baiskeli za zamani zilizoendeshwa kwa farasi, mabaki ya risasi zikiwa zimesamba huku na kule pamoja na mabomu yaliyogandamana.
Pia ndani ya mashimo hayo kuna hospitali ambamo wanajeshi hao walitibiwa, njia fupifupi na vitu vingine vya kivita vikiwa vimeharibika kutokana na kukaa chini ya ardhi kwa muda mrefu.