Na Musa Mateja
KAMA ni kweli manenomaneno yanayozungumzwa mtaani kwamba, mrembo aliyewahi kutikisa kwenye ‘gemu’ la Bongo Fleva, Rehema Chalamilla ‘Ray C’, eti ameanza kubwia ‘unga’ (madawa ya kulevya) kama zamani, basi nyota huyo atakuwa anarudi ‘kuzimu’ ambako alishatoka miaka miwili nyuma, Risasi Jumatano linakupa zaidi.

Hata hivyo, kwa kuweka sawa mzani wa habari hii kama maadili ya uandishi yanavyotaka, gazeti hili liliwasiliana na Ray C ambaye alisema na yeye ameshasikia madai hayo ya kurudia kubwia unga.
TWENDE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Ray C alishindwa na uzalendo hivyo akaamua kurudia kwenye tabia ya kubwia unga kiasi kwamba, hali yake imekuwa si ile ya hapo katikati kwani ameanza kuonekana kuchoka.

Alivyokuwa mwanzo.
AMEACHANA NA DOZI?
Chanzo kikasema: “Hapa ninapoongea na wewe ndugu mwandishi, nina wasiwasi kwamba, Ray C ameacha kutumia dozi na ndiyo maana hali yake si nzuri.”

KAMPANI YAKE KUBWA
Ray C, kwa sasa anatajwa kuwa na kampani ya kijana mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, kwamba ndiye mtu wake wa karibu lakini pia, kijana huyo anasemekana naye ni mtumiaji mzuri wa unga.

CHIMBO
Chanzo kilikwenda mbele zaidi kwa kudai kuwa, maeneo ya nyuma ya Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni, Mwananyamala ndiko kwenye machimbo (anakopenda kushinda) ya mwanadada huyo.

AANZA KUSAKWA RAY C
Kama gazeti hili lilivyosema kwenye aya ya pili kwamba, baada ya kumegewa taarifa hiyo, lilimtafuta Ray C kwa kumtumia meseji kwa njia ya simu ili kumsikia mwenyewe anasema nini juu ya madai hayo.
Risasi Jumatano: “Mambo vipi Ray C?”

Ray C: “Nani mwenzangu?”
Risasi Jumatano lilijitambulisha kwa kutaja jina la mwandishi.
Ray C: “Niambie wangu, tuma meseji kuna ishu ya kitengo nafuatilia kimyakimya, sema.”

Risasi Jumatano: “Kuna taarifa tumeletewa hapa ofisini zinadai kwamba, umerudia tena matumizi ya madawa ya kulevya, sijui ukweli wa taarifa hizi ukoje?”
Ray C: (baada ya muda sana) “upuuzi huo nilishausikia. Nimechoka. Maendeleo yangu anayajua dokta wangu na mimi mkataba wangu na daktari ni very confidential (siri sana). Atakayeongelea matibabu yangu bila kuwa na uhakika basi tutakutana mahakamani. Ninachokifahamu mimi ni kuwa, bado naendelea na tiba yangu.”
AKATAFUTWA RUGE
Risasi Jumatano lilimtafuta Ruge Mutahaba ambaye anatajwa kuwa meneja wa Ray C ili na yeye aseme lolote kuhusu kuwepo kwa madai hayo.

Ruge: “Ni kweli kuna madai Ray C kurudia haya mambo na nimekuwa nikimuonya mara kwa mara, lakini haoneshi kujali wala kubadilika. Nimesota sana kumtafuta lakini amekuwa akinikwepa. Wakati mwingine hapokei simu.
Ruge anaendelea: “Mara ya mwisho alipoona missed call yangu (namba iliyopiga bila kupokelewa) akanipigia simu na kuanza kunitukana sana! Nikashangaa! Hivyo kuanzia siku hiyo mimi nimenawa mikono licha ya kwamba Rais Kikwete ‘JK’ (sasa mstaafu) ndiye aliyenikabidhi huyo mtu nimsaidie, lakini sasa msaidiwaji mwenyewe ndiyo yupo hivyo.”
JK NA RAY C
Desemba 10, 2012, Ray C na mama yake mzazi, Margareth Mtweve walitinga ikulu ili kumshukuru Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ kwa kumsaidia msanii huyo kuondokana na tabu aliyoipata kufuatia kukubuhu katika matumizi ya unga.

JK NA GAZETI LA IJUMAA
JK alichukua umauzi wa kumsaidia Ray C kuhusu matibabu ya kuachana na unga baada ya kusoma habari kwenye gazeti linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers, Ijumaa Toleo namba 799 la Novemba 2-8, 2012 ambalo katika ukurasa wake wa mbele, lilikuwa na habari yenye kichwa; DAH RAY C.

Katika habari hiyo, Ijumaa lilinasa picha ya Ray C akiwa katika hali ya kulemewa na unga akionekana akiwa anauchapa usingizi mzito maeneo ya Magomeni, Dar.