Hans Mloli
Dar es Salaam
SAKATA la Yanga kuvunja mkataba wa kiungo wake mchezeshaji, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima bado halijazima na sasa limechukua sura mpya baada ya kiungo huyo kudaiwa kuanza mikakati ya kujitetea na kuepuka baadhi ya vipengele vinavyombana katika suala la fidia.

Yanga imefafanua kuwa Niyonzima anapaswa kuilipa pia timu hiyo Dola za Marekani 71,175 (zaidi ya shilingi milioni 150) kwa kuwa amekiuka baadhi ya vipengele vya mkataba wake.
Hata hivyo, taarifa zinafafanua kuwa tayari mchezaji huyo ameanza kufuatilia njia za kufuata kwa ajili ya kujinasua na adhabu hizo na juzi usiku alikutana na baadhi ya wadau kwa ajili ya kupanga jinsi ya kuweka mambo sawa huku akifanya vikao usiku mzito.

Championi Jumatano lilimtafuta kwa njia ya simu kiungo huyo ambaye awali alisema hayupo tayari kulipa fidia hiyo, majira ya saa 3.30 usiku kuzungumza naye lakini alipopokea alizungumza machache na kusisitiza kwamba kuna watu anazungumza nao kwenye kikao kifupi hivyo aachwe mpaka baadaye.
“Kama nilivyokwambia lazima nifuatilie hizo pesa nahitajika kuzilipa kwa ajili gani hasa lakini kwa kuwa wameamua hivyo haina tatizo, mpira ni kazi yangu tutaangalia nini kinafuata baada ya hapo ila kwa sasa nipo kwenye kikao kidogo kuna watu nimekutana nao kidogo,” alisema Niyonzima.

Hata hivyo chanzo cha karibu na mchezaji huyo kilisema juzi kuwa mchezaji huyo baada ya kupewa taarifa ya kuachana na timu hiyo alifanya vikao vinne usiku na watu mbalimbali sehemu za Jiji la Dar es Salaam
“Juzi jamaa nilikuwa naye alifanya vikao kama vinne hivi usiku, sikuwa najua anazungumza nini lakini tulikwenda sehemu nne tofauti na akawa anakutana na watu tofauti tofauti,” kilisema chanzo hicho.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo alisema; “Sina la kuzungumzia kwa sasa, bodi imefanya maamuzi na mimi sina la kusema, yeye mwenyewe Haruna anajua alichokifanya.”