Wednesday, December 30, 2015

Jini kabula amwanika wa ubani wake


Miriam-Jolwa-Jini-Kabula1Msanii wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’.
NA gladness mallya
MSANII wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ hivi karibuni alimwanika mpenzi wake kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kuambatanisha na maneno ya kimahaba.
Jini Kabula aliweka picha ya mpenzi wake huyo ambaye hakutaka kumtaja jina huku akiambatanisha na maneno ya kimahaba na alipoulizwa kuhusu suala la ndoa alisema halipo bali ni marafiki tu.
kabula“Huyu ni rafiki yangu sana na niliweka picha tukiwa pamoja kwenye profile yangu na kuandika maneno yale kwa sababu nilijisikia tu kuyaandika, suala la ndoa halipo na wala sifikirii maana maisha haya yenyewe ni ndoa tosha,” alisema Jini Kabula.