Imelda mtema
Ni shedah! Muuza nyago anayeshikilia Taji la The Ijumaa Sexiest Girl 2015, Asha Salum ‘Kidoa’ amefunguka kuwa umbo lake matata linampa wakati mgumu kiasi kwamba hata anapokwenda kutafuta kazi lazima aanze kutanguliziwa kuhusu mambo ya mapenzi, jambo ambalo linamfanya ajichukie.
Kidoa ameliambia Ijumaa Wikienda kuwa kutokana na changamoto anazokutana nazo kupitia umbo lake hilo sasa imemlazimu kuanza mazoezi ili kuweza kujipunguza na kuonekana wa kawaida ili asipate kipindi kigumu katika kutafuta maisha.